Thursday, August 12, 2010

VITUKO VYA MITAANI

2 comments:

  1. 1. Padri alikuwa anafuga kuku, cku 1 Jogoo akapotea. akaamua kutangaza kanisani kwenye ibada
    Padri: wapendwa katika Bwana wangapi wana Jogoo? Wanaume wote wakacmama, Padri: cyo hivyo jamani, namaanisha hivi ni wangapi wameona Jogoo? Wanawake wote wakacmama.
    Padri: Hamjanielewa ni wangapi wamemuona Jogoo wangu? Masista wote wakacmama.
    Padri akatimua mbio..............

    By Susan - WAPI MEMBER


    2.Jamani, mimi nina rafiki yangu tunapendana na kuheshimiana sana. Bwana huyu anapenda sana tutembeleane na kujuliana hali. Kitu kinachonisumbua na kunikosesha raha ni mkewe(yaani shemeji yangu). Mwanzoni ilikuwa kidogokidogo; lakini kwa sasa imezidi kipimo na ninaogopa endapo nitaendelea kuwatembelea kwao nitakuja kupata balaa.



    Mwanzoni ilikuwa kila nikiwatembelea rafiki zangu hawa, jamani jamani zinakuwa nyingi sana kutoka mdomoni mwa shemeji yangu huyu. Kadri siku zilivyokuwa zikiendelea ikawa nikifika mara kanga zidonmdoke, mara maandazi yamponyoke, anakuwa anamaliza kukalia viti vyote na bado hatosheki; kuna siku amevunja seti nzima ya glasi na jagi la juice akachafua sebule nzima. Inakuwa kila anaponiona anahamanika kupita kiasi; mpaka hivi juzi tu alijikwaa mlangoni nusu ya kuvunja meno mmewe akamwuliza "hivi wewe ni vipi ukimwona shemeji yako unakuwa kama umechanganyikiwa ?" Kwa kweli hali hiyo ilinitisha sana.



    Sasa ndugu zangu wana Wapi endapo mna msaada wa kunipa ebu nisaidieni; kama ni kukata mguu nisiitembelee familia hii ama nifanyeje kwa maana shemeji yangu sasa imekuwa TOOOOOO MUCH!

    ReplyDelete
  2. Mtafute huyo shemeji yako private mkae uongee nae akwambie tatizo nini

    ReplyDelete