Ya ilakh hii ndoto, nawaza matafakuri, Nawaza kwenda kushoto, na kulia nakariri, Bado sijaona pato, na mana iliyo nzuri, Ndoto ya maji meupe, kwenye bahari nyeusi.
Naota naogelea, nazama napifa mbizi, Naota nachelelea, kwa mayowe kama chizi, Naota nagugumia, mfano wa dudumizi, Ndoto ya maji meupe, kwenye bahari nyeusi.
Raha ninayo sikia, kwenye bahari nyeusi, Nashindwa kusimulia, kwa lugha ilo nyepesi, Maji haya fikiria, ya kaskazi na kusi, Ndoto ya maji meupe, kwenye bahari nyeusi.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteYa ilakh hii ndoto, nawaza matafakuri,
ReplyDeleteNawaza kwenda kushoto, na kulia nakariri,
Bado sijaona pato, na mana iliyo nzuri,
Ndoto ya maji meupe, kwenye bahari nyeusi.
Naota naogelea, nazama napifa mbizi,
Naota nachelelea, kwa mayowe kama chizi,
Naota nagugumia, mfano wa dudumizi,
Ndoto ya maji meupe, kwenye bahari nyeusi.
Raha ninayo sikia, kwenye bahari nyeusi,
Nashindwa kusimulia, kwa lugha ilo nyepesi,
Maji haya fikiria, ya kaskazi na kusi,
Ndoto ya maji meupe, kwenye bahari nyeusi.